Advertisements

Tuesday, November 24, 2015

MAALIM SEIF NA ZITTO WAMZIKA BI AMINA ABDALLAH AMOUR, MWANAKWEREKWE

Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akitia mchanga katika kaburi la marehemu Bi. Amina Abdallah Amour katika makaburi ya Mwanakwerekwe Zanzibar. Marehemu Bi. Amina ambaye alifariki ghafla jana mchana, aliwahi kuwa Mbunge wa Viti maalum (CUF) katika awamu iliyopita na baadaye kujiunga na Chama Cha ACT-Wazalendo.
Viongozi mbali mbali wa CUF na kiongozi wa ACT Wazalendo Zitto Kabwe (wa tatu kushoto) pamoja na wananchi wakiitikia dua wakati wa mazishi ya marehemu Bi. Amina Abdallah Amour katika makaburi ya Mwanakwerekwe Zanzibar.

Kiongozi wa ACT- Wazalendo Bw. Zitto Kabwe, akitia mchanga katika kaburi la marehemu Bi. Amina Abdallah Amour katika makaburi ya Mwanakwerekwe Zanzibar wakati akishiriki mazishi hayo.

Viongozi mbali mbali wa CUF na kiongozi wa ACT Wazalendo Zitto Kabwe pamoja na wananchi wakishiriki mazishi hayo.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad pamoja na kiongozi wa ACT- Wazalendo Zitto Kabwe, wakiwa katika makaburi ya Mwanakwerekwe Zanzibar kushiriki mazishi hayo.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad akiagana na kiongozi wa ACT- Wazalendo Zitto Kabwe, baada ya kushiriki mazishi ya Mbunge huyo mstaafu wa CUF.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad akiwapungia mkono wananchi katika mtaa wa Mwembe Tanga Zanzibar, katika hafla ya mazishi ya Mbunge huyo Mstaafu wa CUF.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad akisalimiana na kiongozi wa ACT- Wazalendo Zitto Kabwe, alipowasili katika makaburi ya Mwanakwerekwe Zanzibar kushiriki mazishi hayo. (Picha na Salmin Said, OMKR)

No comments: