Advertisements

Saturday, October 3, 2015

Wasanii wametuangusha kabisa uchaguzi wa mwaka huu

2 comments:

Unknown said...

Sio wasanii waliowaangusha watanzani bali ni chadema na ukawa kwa kumuengua Dk Slaa kwenye ticket ya kugombea uraisi na badala yake kumsimamisha mgombea ambae watanzania wote wanamfahamu kuwa ni fisadi. Dk Slaa ni kipenzi cha kweli cha wale wote waliokuwa wanataka mabadiliko ya kweli. Sasa leo kuwashushia lawama wasanii ni upuuzi mtupu. Nchi hii hayatizamwi maslahi ya wasanii peke yao bali yanatizamwa maslahi ya watanzania wote,maslahi ya taifa zima . CCM walipoamua kumuengua Eduwadi lowasa kwa kweli walifanya maamuzi mazito mno. Walifanya maamuzi hayo kwa kuzingatia maslahi ya Taifa zaidi kuliko chama chao na walistahiki kuungwa mkono kwa kila hali. Tofauti na chadema na ukawa walifanya maamuzi ya kumtimua Dk Slaa na kumleta Lowasa kwa kuzingatia maslahi ya chama chao kuliko maslahi ya Taifa na watanzania. Sasa utaona wasanii ni wa kupongezwa sana kwa kuwaelimisha watanzania kuweka maslahi ya Taifa kwanza kuliko ya taasisi au mtu binafsi. Na kwa kweli kila anampendekeza magufuli kuwa raisi ni mtu ambae anaeweka maslahi ya Taifa na watanzania kwanza kwa kuwa bila ya ubishi magufuli siku zote amekuwa ni mtu mweye kuweka maslahi ya Taifa na watanzania kwanza katika maisha yake yote ya kazi. Mungu ibariki Tanzania yetu. Ameen

Anonymous said...

Bila ushabiki wa kisiasa usiokuwa na tija, ulichosema mdau hakina ubishi na kinasimama kwa miguu yake chenyewe!