Advertisements

Monday, August 31, 2015

TAARIFA YA NDUGU JOSEPH MUNGAI KUHUSU UJENZI WA SHULE ZA KATA NA CHUO KIKUU CHA UDOM. 5/3/2015:

Sijawahi kuona tangu nizaliwe kuona baadhi ya watu wana mawazo ya mgando na akili ya kusahau lini Lowassa alijenga shule za kata? Mimi ndiye nilikuwa waziri wa elimu na utamaduni kwa miaka miaka minane.

Shule za sekondari za kata zilijengwa na nguvu za wananchi wenyewe serikali ya awamu ya Tatu chini ya Rais Benjamin W. Mkapa ndio ilihamazisha kila kata nchini nzima kuwe na sekondari waziri wa elimu nikiwa mimi Joseph Mungai.

Nikiwa waziri wa elimu na utamaduni wakati huo niliteua kikosi kazi kila mkoa wakuu wa mikoa niliwaagiza kuwahamazisha wananchi kila kata kujenga shule za kata ndio maana baadhi ya shule zingine za kata ziliitwa majina ya wakuuu wa mikoa.

Wakati Benjamin W. Mkapa mkapa hajamali muda wake wa uongozi alifungua shule za kata nyingi sana nchi nzima shule zingine aliziwekea mawe ya msingi akiwepo waziri mkuu Sumaye naye alifungua shule hizo za kata nikiwepo mimi nilifungua shule hizo nikiwa waziri wa elimu na utamaduni.
Kipindi hicho Lowassa akiwa waziri wa maji na mifugo wakati Rais kikwete anaingia madarakani mwaka 2005 alikuta shule za kata nchi nzima zikiendelea kujengwa kwa nguvu za wananchi wenyewe walijitolea.

Leo hii Lowassa anawadanganya wananchi alijenga shule za sekondari za kata anawatuma vibaraka wasema yeye ndiye alijenga shule za kata wakati tulioshiriki na ujenzi wa shule za kata tupo tukae kimya siwezi kukaa kimya lazima nisema ukweli Lowassa hakujenga shule za kata.
Watanzania kuweni macho na wasaka urais maendeleo yote serikali ndio inayafanya kwa kodi zenu.

Kuna watu kwenye mitandao ya kijamii wanatumika kumsafisha Lowassa mtu kibaka mtu mchafu mwenye matongo tongo ya kila aina ya uchafu mwl. Nyerere aliwahi kusema mtu kipofu mwenye kichwa kikubwa ndani ya kichwa chake hakuna akili mtu huyo hawezi kuona wizi wa Lowassa.

Wapo baadhi ya watu wanasema Lowassa alijenga chuo kikuu cha Dodoma chuo gani hicho Lowassa alijenga?
Wakati wa ujenzi wa chuo kikuu cha Dodoma mimi na waziri wa elimu ya juu wakati huo Piyusi Ng'wandu tuliitwa IKULU na Rais mkapa alituambia tutafuta eneo la ujenzi wa chuo Kikuu Dodoma kesho yake tulienda Dodoma tulikutana na wanakijiji wa maeneo hayo kilipojengwa chuo hicho.

Wananchi walikubali kuyaachi maeneo hayo malipo yalifanyika kila mwenye eneo alilipwa na serikali ujenzi wa chuo hicho ulianza kufyeka misitu baadhi ya sehemu serikali ilisimamisha ujenzi ili upite kwanza uchaguzi mkuu ndio uliomweka madarakani Rais kikwete

Bajeti iliyokuwa imepangwa kunza ujenzi wa chuo kikuu cha Dodoma ilitumika kujenga nyumba ya Rais mstafu alikuwa anaondoka IKULU muda wake wa uongozi ulikuwa umeshaisha na kumalizia ujenzi wa ukumbi wa BUNGE Lowassa akiwa waziri wa maji na mifugo.

Nashangaa sana kumeibuka kikundi cha watu wachache kinasifia mabwana wasaka urais badala ya kuisifia serikali au Rais aliyewaletea maendeleo wananchi eti Lowassa alijenga shule za kata mara alijenga chuo kikuu mara alipeleka maji miji ya shinyanga na Kahama poleni kwa kudanganywa.

Nawaomba sana wale wanaomnadi Lowassa watafute njia nyingine ya kumnadi waache kabisa kusema Lowassa alijenga shule za kata na chuo kikuu cha Dodoma ni mimi na wenzangu ndio tuliofanya kazi hiyo ya ujenzi sio Lowassa.

Kesho ataibuka waziri Magufuli atasema amejenga barabara kesho ataibuka mhe. Kapuya atasema amejenga uwanja mkuu wa mpira jijini dar es Salaam wakati huo kapuya alikuwa waziri wa michezo kesho ataibuka waziri mwakyembe atasema amejenga viwanja vya ndege.

Siku ikifika nitazunguka nchi nzima kuueleza umma wa watanzania mimi ndiye Joseph Mungai ndiye niliyeshiriki ujenzi wa shule za kata nchi nzima Rais wangu akiwa Mkapa sio Lowassa Rais ajaye Mungu anamjua sana.

Namjua sana Lowassa kama kidole changu nimefanya naye kazi kwa karibu sana hafai kuwa Rais hata nafasi ya waziri mkuu hafai sina ugomvi na Lowassa namshauri apumzike siasa kama nilivyopumzika mimi awaachie wengine waadilifu.

Chanzo cha taarifa:
Mafinga Online: Joseph Mungai amshauri Lowassa apumzike siasa, asema anamfahamu lowasa kama kidole chake..

3 comments:

Anonymous said...

Haaaa Mungai mweleze Mungu tu ndio atayasikiliza malalamiko yako huna maana mtandaoni hakuna wa kukusaidia sawa mzee

Anonymous said...

Yeyote aliyepost hii article ni nyang'au. ... Joseph mungai leo hii alikuwepo kwenye mkutano wa ukawa,na alikaa meza moja na mh,Lowassa. Sasa haya maneno mnayatoa wapi?

Anonymous said...

Tatizo kubwa hapa ni siasa uchwara na kuona fulani hafai wakati hao walioko humo ndani ni wachafu vibaya mno. Nchi inatafunwa na tunaendelea kuona fulani fulani kwani chama ni kimoja tu mbona vipo vingi na hatuni mabaya yanayoandikwa kuhusu vyama au wagombea fulani au kwa kuwa huyu anakuwa mwiba mchungu kwa chama yetu inayoangamia??? Joseph hebu upumzike kwani uliioeleka elimu mahali pasipofaa na mashule ya binafsi kuibuka sana wazazi wengi hawana uwezo wa kulipa ada kubwa tena kwa elimu ya msingi ambayo ilitakiwa kuwa bure hadi sekondari. Hebu waachwe waTanzania waweke uamuzi mgumu kwanza.