Advertisements

Thursday, July 2, 2015

Ray C : Naomba kuwatangazia kuwa natafuta mchumba wa kuishi naye milele! Atoa vigezo 10 vya mume amtakaye


Msanii wa muziki Rehema Chalamila aka Ray C amefungua mlango kwa mwanaume yoyote anayetaka kumuoa ajitokeze ilimradi awe na vigezo 10 ambavyo ameviainisha.

Kupitia ukurasa wake wa instagram Ray C ameandika:

“Habari zenu wapendwa wote dunia nzima!Leo na habari nzuri sana kwenu,Naomba kuwatangazia kuwa natafuta Mchumba wa kuishi nae milele!nataka niwe nae milele na nimzalie watoto wawili wa kike na wakiume!!!!

Ila naomba niwambie kabisa masharti

1.Awe mpole ili nikikasirika anibembeleze
2.Awe anapenda muvi za kihindi ili nikiwa na stress aniwekee nyimbo za kihindi maana ndio raha ya moyo wangu.
3.Asiwe muongeaji sana sababu huwa sipendi makelele.
4 Anipende na ubonge wangu huu asije akaanza kunambia baby anza mazoezi au dah baby zamani ulikuwa bomba au rudisha kiuno hapo hatutaelewana.
5.Awe ananipikia nikichoka maana navutiwa nikimuona mwanaume anapika.
6.Awe na Mimi muda wote maana na wivu sana ikiwezekana tufanye kazi ofisi moja au awe ofisi ijengwe hapo hapo nyumbani.
7.Awe mvumilivu maana nikiwa na hasira huwa naongea kwa sauti ya juu sana.
8.Asiwe na rafiki wengi,na akitaka kuonana nae na mi niwepo maana si mnajua wanaume tena wakikutana huwa wanashaurina mabaya.
9.Awe anajua nyimbo zangu zote ndio ntaamini kweli ananipenda.
10.Sharti la mwisho kabisa ambalo ni muhimu sana kwangu ni hili tuwe tunatumia simu moja na Namba moja, maana kanisani tunafundishwa kuwa ndoa maana yake tumeungana na kuwa kitu kimoja kwahiyo kama mume na mke tunalala pamoja kitanda kimoja na kuishi pamoja kwanini tusitumie simu moja!Sioni tatizo!

Kama una ndugu,jamaa.kaka,rafiki yuko single basi mjulishe tangazo hili huezi jua unaeza ukashangaa nimekuwa shemeji yako au wifi yako”.

14 comments:

Anonymous said...

Huna mpaango bora ubakie hivyo tu.

Anonymous said...

Ujana umeutumia wapi uzee uwape watu majalibio yako yamoyo.chukuwa kumi zako nenda india kajalibishe.we plaud to be real afrika maandiiingoo (kazi kitandani) kama mdundiko hauwezi kucheza usiingie kati utasukumwa pembeni. punguza sheria upate msitiri ukinichangua mimi wewe utafanya kila kitu hahahaa!

Anonymous said...

Mwanaume hawekewi masharti kama unaanza wewe umepotea.

Anonymous said...

hahahaha...hilo la makelele hata mimi silipendi, unakuta mwanaume anaongea hadi masikio yanaziba kwa makelele!

Anonymous said...

Aka, mimi hapana taka yeye; nisijefundishwa kubwiya unga bure!

Anonymous said...

Hukupata wa kukusetiri moyo wako miaka nenda hadi umechoka sasa unatoa masharti. Waulize walioko kwenye ndoa wakujuze! hayo yote unayotaka je wewe unayaweza?? sidhani kama kuna mtu anayetaka kuwekewa masharti ndoa ni maelewano ikikushinda unasepa!! Kwa mtaji huu sidhani kama unaweza kudumu hata kwa miezi mitano!!. pole weeehhhh.

Anonymous said...

Hueleweki wewe, angalia No. 7 na No. 3, huwezi chukia kelele halafu ukawa unapiga kelele!!!

Anonymous said...

mummy muombe mungu utampata tu na atakutimizia masharti yako hayo yote na zaidi ya hayo amini mungu sema naye kwa moyo wako wote kila leo kila siku ibada ni hiyo hiyo tu muombe na muambiye mungu masharti unayoyataka ndo hayo utampata tu aminia wangu.

achana nao watoa comment hapo juu hakuna kama mungu hata siku mmoja wasikubeze bure na mimi naona ni masharti madogo sana hayo;ungeongeza na ziada.

mimi ningekuwa niko free ningekuja kukuchukua jumla jumla;tena ningekuja kukuambia uongeze masharti yako.naona ni kidogo sana si siri na wala si kuthihaki iam serious.sema tena ndo ninaye wangu tena namfanyia zaidi ya hayo.

nimezaliwa mwanamme peke yangu na nina dada wengi tu so najua hisia za mwanammke na najua sana kupeti peti wala sioni tabu kumpa raha mpenzi wangu ajisikiye na adeke deke kwa malove davi yangu.

na sisitiza muombe mungu sana kwa hayo masharti yako na muachiye yeye atakupa yote uyatakayo na zaidi.amen.

candlestudios said...

Naamini Mungu atakujalia utampata tena kuna wanaume ambao hawataki mwanamke Awe kimbaumbau (mwembamba) wanataka Turbo (bongebonge) Naamini Mungu ni mwaminifu Ukimwomba atakufanikishia hitaji la Moyo wako Kwa Muda utaofaa Najua uko makini maana na huku Mtandaoni kuna maigizo.

Unknown said...

Nicheki in box 0715772511

Unknown said...

Nitafute mama tuyajenge,ila mm mjacriamalitu(Fundi)

Unknown said...

Nicheki

Unknown said...

Nitafute bibie

Unknown said...

Mm nipo tayary