Advertisements

Monday, June 29, 2015

WATANZANIA WAISHIO NEW YORK NA MIJI JIRANI WASHIKAMANA NA KUMZIKA MZEE ALFRED MAGEGE


Mzee Magege  apumzishwa kwenye nyumba yake ya milele kwa ushirikiano wa jumuiya ya Watanzania waishio New York na miji ya jirani. Sala ya kumuombea mzee magege na kuaga mwili wake vyote vilifanyika Victory Seventh-Day Adventist Church Bronx. Ny. na kisha kumsindikiza kwenye nyumba yake ya milele huko Mount Prospect Cemetery Neptune City. Nj.

 Mwili wa mzee Magege ukiwa ndani ya jeneza tayari kwa kuifadhiwa kwenye nyumba yake ya milele.
 Mke wa marehemu akiwa na watoto wake mbele ya nyumba ya milele ya marehemu mume wake

Familia ya marehemu mzee Magege wakipata picha ya kumbukumbu 

 Watanzania wakiwa makaburini kushuudia mwili wa mzee Magege ulivyokuwa unapumzishwa kwenye nyumba yake ya milele.

Familia ya marehemu  watoto na wajukuu wakiwa kanisani 

 Mke wa marehemu Mzee Magege akiwa na watoto wake 

 Watoto wa marehemu

 Kwa picha zaidi ya shughuri mzima nenda soma zaida 



Familia ya mzee Alfred Magege wakipata picha ya pamoja mbele ya kaburi lake baada ya kuitimisha safari ya kwenye nyumba yake ya milele. Matukio zaidi tembelea website hii http://tembaphoto.com/index.php?sphoto=1

4 comments:

Anonymous said...

poleni sana wafiwa. ila watu wanao-smile kwenye msiba huwa siwaelewi kabisaa

Anicetus said...

Sabababu ya msiba ni kukutanisha watu, na watu wakikutana wanakuwa na na furaha na mambo mengine yanatokea

Anonymous said...

Poleni kwa msiba kwa wanafamilia na marafiki kwa ujumla...Mungu awatie nguvu katika kipindi hichi kigumu mnacho kipitia.

kwa uliye andika hapo juu....
Huwezi kuelewa kwanini watu wanatabasamu kwenye picha sababu kila mtu ana jinsi ya kipekee ya kuomboleza katika msiba. Kila mtu anaujua moyo wake binafsi na majonzi pia..sentensi yako ya kwanza ilikua imejitosheleza...

dorice said...

Poleni sana wanafamilia Mungu awatie nguvu na ailaze roho ya baba yetu mahala pema peponi.Amina