Advertisements

Friday, May 29, 2015

UMAARUFU WA RAMADHANI SINGANO NA MAHALI ANAPOISHI HAVIFANANI KABISA!

HILI NDIYO CHOCHI ANALOPITIA SINGANO MCHEZAJI MAARUFU WA SIMBA KUELEKEA KWENYE CHUMBA ANACHOLALA. YANI USINGIZI WA MCHEZAJI HUYO KIPENZI CHA WAPENZI WA TIMU MAARUFU YA SIMBA NDIYO HAPA. JITIRIRISHE HAPA CHINI UONE NDANI YA CHUMBA NA MAISHA YAKE KWA UFUPI TU. HAPO NDIPO UTAKUBARI KUWA MPIRA WA BONGO NI NYOKO NA UMBUMBU WA KUTOJITAMBUA KWA WACHEZAJI WA TANZANIA. NA UCHWARA WA UKILAZA WA WA VIONGOZI WA TIMU ZOTE ZA TANZANIA
Chumba anacholala Singano na Kaka yake Hais Ramadhani
UMAARUFU ni kama utumwa! huwezi kuwa huru kama una jina kubwa, halafu maisha yako ni ya kawaida tu.
Kuna idadi kubwa ya wachezaji maarufu wa mpira wa mguu nchini, pia wapo wanamuziki n.k, lakini maisha wanayoishi ni tofauti na majina yao. Ni maisha ya kiwango cha chini.
Katika soka la Bongo, huwezi kutaja wachezaji wenye majina makubwa kwasasa ukaliacha jina la Ramadhani Singano ‘Messi’.
Singano akiwa na majirani zake
Uwezo wa kupiga chenga, pasi, kasi na staili yake ya uchezaji ya kutumia mguu wa kushoto akitokea winga ya kulia ni vitu vinavyofanya Singano aonekana mahiri kusakata kabumbu.
Kila mtu kwasasa anajua kwamba Singano ana matatizo ya kimkataba na klabu yake ya Simba na tulieleza kwa undani siku ya jana.(Rejea habari za jana).
Katika stori yetu ‘exclusive’ na Singano jana, tuliahidi kuendelea na sinema ya suala lake na leo tunakuletea sehemu ya pili ya maisha yake binafsi.
Singano anaishi kwa ndugu yake eneo la Keko, Machungwa jijini Dar es salaam.
Kiukweli; maisha anayoishi Singano yanasikitisha mno, hana nyumba, badala yake ameomba hifadhi kwa kaka yake, Hamis Ramadhani ambaye pia anamsimamia mambo yake (Meneja).
Hamis na Singano ni ndugu wa damu, wamezaliwa na mama mmoja baba tofauti.
Baadhi ya picha za ukutani chumbani kwa Singano
Moja ya vipengele katika mkataba wa Singano ni kupatiwa kodi ya nyumba, lakini katika maisha yake yote toka asaini mkataba huo Mei 1, 2013 hajawahi kupewa hata shilingi kama anavyothibitisha mwenyewe; 
“Kipengele cha kulipiwa kodi ya nyumba hakijatekelezwa, niliuandikia barua uongozi wa Aden Rage toka mwaka jana, lakini mpaka sasa naona kimya. Nashangaa kitu kimoja; uongozi huu wa Rais Aveva (Evans) baada ya kuingia madarakani unasema ulipokea nyaraka zote, sasa vipi barua yangu ya kudai stahiki zangu hawakupewa au hawajaiona?”
SWALI: Singano, mtandao wetu umefika unapoishi hapa Keko -Machungwa na kushuhudia maisha yako halisi, dhahiri mazingira haya hayafanani na umaarufu wako, unaishi chumba kimoja na kaka yako wakati kuna kipengele cha kupewa kodi ya nyumba na hukijatimizwa, una lipi la kuwaambia Wachezaji wa Kitanzania na Watanzania wote?.
Singano: “Mimi kidogo nipo tofauti na wengine, kwanza kabisa wanichukulie mtu wa kawaida, wasiamini kile wanachokiona kwenye magazeti au media. 
Kwa jina langu mimi Ramadhani Singano Messi watu wanaweza kutegemea naishi vizuri, maisha ya hali juu, hapana! siwezi kuigiza, maisha yangu ni ya chini sana.
Naishi kawaida sana, nikiamka asubuhi naenda kuswali, nikirudi nakaa nyumbani tu. Chumba tunalala chumba kimoja na kaka yangu, wakati kwenye mkataba wamesemanitalipiwa nyumba. Nimeomba hifadhi kwa kaka yangu. Labda watu watahisi kuna watu wananitumia, hapana!, ninadai haki zangu, tuweke sawa mambo ya kimkataba ili niwe huru na kuendelea kuongea na klabu yeyote”.
Kwa mazingira anayoishi Singano na wengine wengi, ni wazi kwamba wachezaji kibao wanajikuta wanashuka kiwango bila sababu. 
Mchezaji hawezi kuwa huru, hawezi kuwa sawa kisaikolojia , muda wote anawaza namna ya kuikabili presha ya watu.
Kila mtu anamjua na wengine wanahitaji kumtembelea nyumbani kwasababu ni marafiki wa kimpira, wanamheshimu sana, lakini anapoishi hapana hadhi kabisa, hivyo anaogopa kuwakaribisha moja kwa moja. Utacheza vizuri kwa wakati wote?
CREDIT:SHAFFIHDAUDA

No comments: