Advertisements

Friday, December 26, 2014

AINA 10 ZA WANAWAKE WANAOPENDWA NA SANA NA WANAUME

WAPENDA USAWAAina ya pili inayohitajika katika katika ulimwengu wa kimapenzi niwanawake wanaoheshimu usawa wa jinsia, walio tayari kubeba majukumu yakifamilia kwa ulinganifu sawa na wanaume, wenye uwezo wa kuongoza jamiikwa asilimia 50 kwa 50
WANAOJUA MAPENZIWanawake wajuzi wa mambo ya faragha wanapendwa sana. Sifa yao kubwa niuwezo wa kuwatosheleza wenzi wao katika tendo la ndoa. Tafiti zinaonesha kuwa wanaume hupenda sana wanawake watundu katika mchezo wa sita kwasita. Mara nyingi wanatajwa kuwa na uwezo wa kuteka akili za wanaumebila kujali sifa zao za nje au za ndani 


MARAFIKI Wanawake wenye sifa sawa na rafiki ni aina ya nne inayowavutia wanaume.Wao hutegemea zaidi nguvu ya kushawishi inayotokana na namna wanavyojali na kujitolea kuhakikisha wanakuwa marafiki wa kweli kwenye shida naraha kwa wapenzi wao. Si wakorofi, ni waungwana na wapenda amani 


WAPENDA UWAZI Aina nyingine ya wanawake inayowavutia wanaume ni wenye msimamo nawapenda uwazi. Si wepesi wa kuburuzwa katika maamuzi ya msingi kwakisingizio cha wao ni wanawake. Utafiti unaonesha wanawake wa aina hiiwamekuwa muhimu hasa kwa wanaume wenye tabia za ubabe na udhaifu katikauelewa wa mambo. 


WANAOJITEGEMEA Wanawake wanaojitegemea wana soko kubwa kwa wanaume tofauti na akina‘naomba vocha’ kila siku. Uchunguzi unaonesha kuwa wanaume wa leohawapendi wanawake tegemezi, wasiokuwa na kazi na wanaoendekeza stareheza upande mmoja. 


WASIO NA PRESHANikisema wanawake wasiokuwa na presha namaanisha wasiolazimisha vituvitokee haraka haraka. Wao siku zote huacha mambo yatokee yenyewe nakazi yao kuwa ni kutenda sehemu ya majukumu yao kama wapenzi

MARIDADI Kundi lingine la wanawake wanaopendwa na wanaume ni wanaozingatia usafina kujiremba. Wanaokwenda na wakati katika mavazi na mvuto wa nje lakini pia ni waelewa wa mazingira, si washamba. Wanapendeza kwa mwonekano. 

WANAORIDHIKA Wanawake ambao huridhika na hali walizonazo ni kivutio kikubwa kwawanaume. Hili ni kundi linalohitajika sana katika ulimwengu wa mapenzikwa upande wa wanaume ambao maisha ya sasa yamekuwa yakiwageuza kutokajuu kwenda chini au chini juu. Kukubali hali zote bila kubadili tabia ni sifa njema ya mwanamke 

WA MMOJA Wanawake wanaochagua mara moja na kutosheka na kuwa tayari kukwepa kilaaina ya vishawishi toka kwa wanaume ambao kimtazamo wana vitu vya ziadazaidi ya waliowachagua mwanzo, wanahitajika sana.“Niliye naye ananitosheleza kwa kila kitu sitaki mtu mwingine.”Kundi la wanawake wa aina hii ni adimu na muhimu sana.
CREDIT:DODOMA CLAN

11 comments:

Anonymous said...

Ndugu yangu, tupo ila tunaangukia mikononi mwa wanaume wasiojua thamani zetu!

Mlay said...

Na wanaume je? Wanayo pia hizo sifaaaa? It should be both ways sio mwanamke peke yake. Mwana ume pia anatakiwa ku deliver

DavePK said...

100%

Anonymous said...

Mdau, kama mnaangukia mikononi mwa wasiojua thamani zenu inawezekana nyie wenyewe mnakuwa hamjui thamani zenu au mnachokitaka!

DavePK said...

100% not 50%

Anonymous said...

kwani uangukiye kwenye mikono ya mwanamme asiyejua thamani zenu?

kama huwezi kujithamini wewe hakuna atakaye weza kukuthamini wanaume wapo tafauti wote si sawa tupo tunaothamini sana wanawake na pia kujua kuwalea kimapemzi ukiona huyo mwanamme uliye yane hakuthamini KIMBIA,Sitaki kukutenganisha na ndoa yako ila lazima ujuwe kuthaminiwa ni muhimu anza kwako mwenyewe kujithamini na ukiwa na CONFIDENCE hakuna mwanamme yeyote atakaye kuchezea chezea ovyoo.mwenyewe tu akikuona una Confidence na unajipenda na kujithamini ata uFYATA MKIA WAKE na ndo hapo penzi litakapo chipuka.

wanaume huwa wanaogopa sana wanawake walio indepedecy kwa mapugufu yao but hawajui mwanamke namna hiyo ndo poa sana.

Dunia hii ya leo ni yenu kina mama usisikiye don't ndo maana kuna baadhi ya wanaume wanajua hilo kwa HOFU ZAO wanakandamiza wanawake

BILA YA NYINYI SISI HATUWEZI KUMBUK HILO MUMMY.TUNA NGUVU TU ZA KIMWILI BUT NOT KWA KILA KITU KAMA MLIVYO NYINYI WASTAHAMILIVU WENYE UPENDO WA KWELI NA HESHIMA.

jithamini mama usingoje mwanamme akuthamini hatokuthamini kama huwezi kujithamini atakutoa thamani na kamwe usikubali hilo okay mummy. HAPPY NEW YEAR

Anonymous said...

Mdau hapo juu umesema kweli kabisa, yupo wenye sifa karibu zote hapo juu, lkn aina ya watu tulionao hawazioni,sijui Ni dharau, yaani nakosa jinsi ya kuwaita, mpaka mtu unakata tamaa. Mweeee.

Anonymous said...

Dunia ya mapenzi imetawaliwa na Ibilisi,,kwahiyo Waweza kuwa na sifa hizo na zisionekane kwa wanaume.Nadhani umesahau swali muhimu la uchamungu.kuelewa maagizo ya mungu na makatazo yake. B

msema kweli said...

Ndugu yangu umesahau jambo la muhimu sana la uchamungu ,,unaweza ukawa na sifa zote hizo lakini kwakuwa tuko kwenye dunia ya ibilisi ni Kazi sana kujua umuhimu wa mwanamke.

Anonymous said...

Wanaume wanakimbilia wazungu. Wanaacha wa kwao. Sijui ndio wenye sifa hizo?

Anonymous said...

wazungu hawana sifa hizo wanakimbilia huko kwa sababu wazungu watawapa makaratasi rahisi hawana mabwana wanaasaka hao mabwana na akija kitu cha dude jeusi jeusi anapata karatasi kilaini ndo hao wanawakimbilia wazungu.
La pili wazungu hawana mdomo mdomo sana kama ma baby wetu wa kibongo kila kitu kwake pao poa so unawez uka cheat na mzungu akausamehe kwa mbongo mwenzetu KITAWAKA/KITANUKA NA UTATAMANI ARDHI IPASUKE.
wazungu wanajua kujipendekeza atafanya kazi yeye nakulipa nusu kwa nusu kodi ya nyumba ya gari na watoto kuwaangalia ki fedha etc na atampa pia pocket MONEY mumewe kama akimwambia baby leo sina mimi,mbongo mwenzako THUBUTU kama hujipendi mwambiye hiyo na akikupa ujuwe kishawahadithia mashosti wenzake, mwenzenu yule ananiombaga fedha kila leo hata Dolla irishirini hana mfukoni mwanamme yule mmh naishi naye tu nina matatizo kweli hanihudumii etc.

Yapo mengi but hayo ndo yanayowafanya wanaume wa kitanzania WAKIMBILIYE WAZUNGU.

Usikate tamaa baby sisi tupo tu tunaojua kupenda na kuthamini vya kwetu nyumbani tutafute utatupata usikate tamaa nakuomba jambo hilo.na najua you must be so cute na mwenye heshima sana.

usimsahau mungu muombe sana atakusaidia kwa yote maana hakuna kama yeye hakuna yeye anachokishindwa ni yeye peke yake hana msaidizi ni mungu mmoja muombe kwa moyo wako wote atakusaidia na utakuja pata faraja ya moyo wako.Ameeen.