Advertisements

Sunday, November 23, 2014

KIJANA SANDE ALIYEKUWA NA KILO 250, AMEFARIKI DUNIA NA KUZIKWA JANA

Kijana Sande Mrema aliyekuwa na tatizo la kuwa na kilo nyingi zilizokuwa zikifikia 250 na umri wa miaka 25 aliyekuwa eneo la Karakana katika moja ya Hoteli alipokuwa akiishi wakati akisubiri kupatikana kwa Ndege amefariki dunia usiku wa saa nne kuamkia Jumamosi Novemba 22, 2014 jijini Dar es salaam.
Sande amefariki dunia wakati bado taratibu za kuona ni namna gani atakavyoweza kupatiwa ndege kwaajili ya kwenda kupatiwa matibabu nchini india zilikuwa zikifanyika miongoni mwa wanandugu.
Sande Mrema alishindwa kusafiri kwenda nchini india katika matibabu yake baada ya kushushwa mara kadhaa kwenye ndege za kimataifa anazotakiwa kusafiria licha ya ndugu zake kulipa Gharama zote za usafiri wake.

No comments: