Advertisements

Friday, September 12, 2014

DIVA ATOA YA MOYONI KUWA ZITO KABWE NI MUME WAKE KISHERIA SOMA HAPA

MTANGAZAJI wa Kipindi cha Ala za Roho kinachorushwa kupitia Radio Clouds FM ya jijini Dar, Loveness Malinzi ‘Diva’ kwa mara ya kwanza, amejilipua kuzungumzia uhusiano wake na Zitto Kabwe kwamba walikuwa mke na mume.
Mtangazaji wa Kipindi cha Ala za Roho, Loveness Malinzi ‘Diva’ akipozi.
Katika mahojiano maalum na mwanahabari wetu jijini Dar juzi, Diva alisema anashangazwa na baadhi ya vyombo vya habari (siyo vya Global Publishers) kumnyima uhuru wa kuongelea suala lake na ‘zilipendwa’ wake huyo wakati kisheria yeye ni mke wake hivyo anapaswa kuzungumzia kutengana kwao.
MSIKIE DIVA
“Ninyi mnayaongelea mambo ya Zitto na mimi juu kwa juu tu hamjui kama mimi nimeishi naye kama mke na mume nyumbani kwake Masaki (Dar), sasa nini kilisababisha penzi letu kuvunjika watu hawajui, nina ushahidi wa kutosha lakini wanaongeaongea tu,” alisema Diva.Akaongeza: “Sasa ninavyojua mimi kwa sheria za nchi, mwanamke na mwanaume wakiishi pamoja kwa zaidi ya miezi sita tayari ni mke na mume. Hawezi kuniacha kirahisirahisi tu.”
KIPINDI CHAZUA BALAA
Diva alikwenda mbele zaidi kufuatia kauli ya Zitto aliyoitoa hivi karibuni kupitia Kipindi cha Mkasi kinachorushwa hewani na Runinga ya East African Television ‘EATV’ na mtangazaji Salama Jabir.
Zitto aliulizwa ana uhusiano gani na Diva, naye akajibu ni mtu wanayefahamiana tu lakini si mpenzi wake.
Mh. Zitto Kabwe akiwa kazini.
HASIRA ZA DIVA
Ilidaiwa kwamba, majibu hayo ya Zitto kwa Salama ndiyo yaliyoibua hasira ya Diva hadi kufikia hatua ya kutupia kwenye ukurasa wake wa Instagram, e-mail aliyodai aliwahi kutumiwa na Zitto siku za nyuma akimtaka asiwe anaweka wazi uhusiano wao kwa sababu atachafuka kisiasa.
E-MAIL ILIVYOSOMEKA:
“Unanikosea sana ujue unapoweka mambo yetu hadharani. Ninaonekana siwezi kuwa kiongozi kwa sababu nashindwa ku-handle masuala yangu binafsi.
“Madhara uliyoyafanya ni makubwa sana. Wapinzani wangu wa kisiasa watayatumia sana dhidi yangu.
“Ungekuwa unajua madhara yake usingethubutu kufanya ulivyofanya mara tatu sasa. Sijui nia yako nini, ila ipo siku utajua umenikosea sanasana.”
SWALI LA MWANDISHI
Je, Zitto akikubali kufuata huo utaratibu uwe mkewe utamuacha GK ambaye umekuwa ukimtangaza kuwa mpenzi wako?
Diva: Hilo nitakujibu baadaye.
SIKU ZA KARIBUNI
Siku za karibuni, baadhi ya vyombo vya habari vimekuwa vikiripoti uhusiano wa Diva na Zitto bila kuzama kwa undani.KUHUSU DIVA
Kufuatia Diva kutupia madai hayo mtandaoni na kudai yeye ana hadhi ya mke kwa Zitto na kauli ya Zitto kwenye runinga kwamba Diva si mpenzi wake, baadhi ya watu waliozungumza na Amani walionesha kwenda kinyume na mtangazaji huyo.
Wengi walidai kwamba wana kumbukumbu zilizonyooka kwamba Diva amewahi kujinadi kutoka na Mbongo Fleva, Gwamaka Kaihula ‘Crazy GK’.“Sasa Diva anavyodai ni kama mke wa Zitto mbona anamtangaza mwanaume mwingine?” Alisema mkazi mmoja wa jiji aitwaye Yuda.
Naye Ismail Juma, mkazi wa Kigogo, Dar alisema aliwahi kusoma kwenye vyombo vya habari kwamba Diva anapumzika na mwanamuziki kutoka Kenya, Jackson Makini ‘Prezzo’ kiasi cha kumzalishia bifu na demu wa jamaa huyo, Huddah Monroe.“Diva awe na aibu basi, asikurupuke wakati yeye mwenyewe si msafi kivile,” alisema Ismail.
ZITTO ASAKWA
Kufuatia madai hayo, kwa muda wa siku saba, Amani limekuwa likimsaka Zitto kwa njia ya simu lakini bila mafanikio.Watu wa karibu naye walipoulizwa alipo, walisema wanachojua ana shughuli zake nchini Zambia.
Ilibidi Amani limtumie e-mail na kumuuliza anachosema kuhusu madai ya Diva lakini kwa zaidi ya siku kumi sasa hajajibu chochote licha ya kumfikia.E-mail iliyotumwa kwa Zitto, Septemba 2, mwaka huu ilikuwa na kichwa cha utambulisho kisemacho; Mambo ya Diva.
E-mail yenyewe iliandikwa hivi: A. Alaykum,

issues za Diva zimekuwepo muda mrefu sasa. Mitandaoni hali inazidi kuwa mbaya. Nimeshasimamisha stori isiandikwe ili useme mpaka naonekana adui wa habari.Naomba uzungumze kitu tuone inakuwaje hii kitu kusafisha atmosphere (upepo). Kukaa kimya si suluhu.
(jina la mwandishi).

2 comments:

Anonymous said...

Hivi huyo anayejiita diva kichwa change kiko sawa?maana anatafuta kiki kwa nguvu kutwa anaongea upuuzi,kwanza huna hata mvuto undo maana unaongea ongea ovyo ukipata mwanaume

Anonymous said...

acheni chuki binafsi hizo kwa kusema huyu demu hana mvuto labda mlitongoza mkatolewa nje sasa kuzima makali ya moyo wenu mnapakazia ....
baby sexy kama huyu hanamvuta labda wewe si rijali.