Advertisements

Saturday, July 26, 2014

MALI ZA BILIONEA ZAZUA TAFRANI BAADA YA KUFARIKI DUNIA

 Moja ya magari ya Bilionea

Nyumba ya Bilionea

Deogratius Mongela na Chande Abdallah
DUNIA haina huruma! Siku mbili baada ya kumzika mumewe ambaye alikuwa bilionea maarufu Dar, Amir Tabu, mjane wake, Mwanahamis Rajab ameingia kwenye tafrani kubwa na mashemeji zake kisa, mali za marehemu huku akitimuliwa kwenye nyumba aliyokuwa akiishi na mumewe.

Tukio hilo la kusikitisha lililoshuhudiwa na wanahabari wetu lilijiri mapema wiki hii nyumbani kwa mjane huyo, Mbezi-Beach, Dar ambapo kulikuwa na kikao cha familia, yaani upande wa mume na mke.

Gazeti hili lilijipenyeza ‘kikachero’ kwenye kikao hicho na kushuhudia mzozo mkubwa kwa upande wa ndugu wa mume wakimtaka mfiwa atoke kwenye nyumba aliyokuwa akiishi na kumtaka kwenda kukaa kwenye nyumba yao nyingine iliyopo Bagamoyo, jambo ambalo lilipingwa vikali na upande wa pili hivyo kuzuka malumbano mazito hadi kikao kuvunjika.


MJANE ANENA
Akizungumza na wanahabari wetu, mjane Mwanahamis alielezea mkasa mzima namna ambavyo ndugu wa mumewe walivyojiandaa kumdhulumu mali alizochuma na mumewe.

Alisimulia kwa uchungu: “Mimi na Tabu tulifunga ndoa halali mwaka 2005. Nakaribia miaka 10 sasa katika ndoa yangu japo sikubahatika kupata mtoto lakini nilimkuta mume wangu akiwa na watoto 6.
“Watoto watatu alizaa akiwa kwenye ndoa nyingine na watoto wengine alizaa nje ya ndoa.

“Kwangu, nahesabu watoto wote ni wangu. Hadi tunafikia kwenye haya maisha nimepitia magumu mengi kipindi chote hadi umauti unamkuta mume wangu. “Watoto wake wamekuwa wakiniheshimu kama mama yao, nimemuuguza mume wangu kwa zaidi ya miaka 4 tangu 2010.

“Katika kipindi chote hicho sikuwaona ndugu, walianza kuja baada kuona hali ya mume wangu imekuwa mbaya.“Matatizo ya mume wangu yalianza akiwa kazini kwenye Kampuni ya Toyota. Alikuwa akisumbuliwa na presha ya macho, kisukari na kufeli kwa figo zote.

“Wakati umauti unamkuta, tulikuwa Bagamoyo kwenye nyumba yetu nyingine, huko ndiko chokochoko za dhuluma zilionekana mapema tangu mwanzo kwani ndugu wa mume wangu walikuwa wananizuia kumuona hata mume wangu.

“Waliniwekea masharti utadhani hakuwa mume wangu, niliumia sana.
“Siku moja shemeji yangu mmoja aliniomba aone hati zote za magari ya kisasa, majumba ya kifahari, hoteli, viwanja, bastola, kadi za benki, leseni ya gereji yake iliyopo Magomeni (Dar) na hati ya Hoteli ya Blue Nile iliyopo Bagamoyo.

“Mali zote za marehemu nilikuwa nasimamia mimi. Kulipia ada za watoto shule na matibabu ya mume wangu ila shemeji alivichukua na kukaa navyo, sikujua anataka kufanya nini nashindwa kumwelewa mbona kabla hawakujionesha?“Nitapigania jasho langu na mume wangu hadi tone la mwisho kwani wanataka kunitoa roho kwa presha.”

MAJIRANI WALAANI
Wakizungumza na gazeti hili, majirani wa mjane huyo walilaani vikali kitendo cha ndugu hao wa mume kufanya ukatili huo ambao haukubaliki kwenye jamii.

AFISA MTENDAJI
Akizungumzia ishu hiyo, Afisa Mtendaji wa Kata ya Kawe, Mbezi-Beach B, Hamatton Bhao alisema alipokea malalamiko ya mjane huyo ambapo mdogo wa mjane alimueleza kuhusiana na sakata hilo la ndugu wa mume kutaka kumtoa mjane ndani ya nyumba yake ikiwa ni siku mbili tu tangu amzike mumewe.

Alisema mjane huyo alikuwa akilalamika kudhulumiwa mali alizochuma na mumewe ndipo alipotoa taarifa Kituo cha Polisi cha Kawe baada ya wanadugu wa mume kufika nyumbani kwa mfiwa na kufanya vurugu ambapo polisi walipofika wanandugu walikuwa wameshatimua.
Hata hivyo, polisi waliweka ulinzi wa askari wakiwa na difenda wakiendelea na uchunguzi wa sakata hilo.

GPL

2 comments:

Anonymous said...

ndo maana mwanamkee unatakiwa uwe nacho mwenyewe hata kama ukiwa umeolewa mwambiyie mume akufunguliye biashara au utafute mwenyewe biashara yako siku akiondoka duniania unachako hawakubabaishi hawa mashemeji wenye roho za nyoka

Anonymous said...

Kwa mtazamo wangu naona matatizo haya yanasababishwa na culture yetu ya kutopenda kufanya mambo yetu kwa uwazi,na kwa kuelewa hali halisi kuwa kifo kipo na siku moja tutatangulia mbele ya haki.Kwa kuelewa ukweli huo basi inakuwa ni rahisi kuweka mambo ya miradhi wazi na mapema na hivyo kuondoa chokochoko ya baadhi ya ndungu mara kifo kinapotokea..