Advertisements

Thursday, July 24, 2014

Aliyebadili dini Sudan akutana na Papa

Papa Francis akutana na bi Merian huko Vatican

Mwanamke raia wa Sudan aliyesamehewa adhabu ya kifo baada ya kubadili dini amesafirishwa hadi nchini Italia baada ya kuwa kwenye ubalozi wa Marekani mjini Khartoum kwa zaidi ya mwezi mmoja.

Meriam Yahia Ibrahim Ishag na familia yake waliondoka na ndege ya serikali ya Italia wakiongozana na Waziri wa nchini Italia Lapo Pistelli.

Baada ya kuwasili Italia bi Merian alikutana na Papa Francis ambaye alimsifu kwa kusimamia dini ya ukristu licha ya tishio la mauti.

Merian alikutana na papa katika makao yake rasmi ya Santa Marta iliyoko kwenye makao makuu ya kanisa Katoloki ya Vatican.

Aliyebadili dini Sudan akutana na Papa Francis

Mkutano huo ulidumu kwa takriban nusu saa .

Baba wa Meriam ni muislamu na kwa Misingi ya sheria ya dini hiyo nchini Sudan Meriam pia ni muislamu na hawezi kubadili dini.

Meriam mwenyewe alilelewa na mama yake ambaye ni mkristo na kusema kuwa hajawahi kuwa muislamu.

Aliyebadili dini Sudan akutana na Papa Francis

Pistelli Naibu waziri wa mambo ya nje wa Italia, aliweka picha yake na Meriam kwenye ukurasa wake wa facebook akisema kuwa wanaelekea kutua mjini Roma.

Mume wa Meriam Daniel Wani, ni mkristo,ana asili ya Sudani kusini na ana uraia wa Marekani.

Mtoto wa Meriam, Maya alizaliwa gerezani mwezi May, muda mfupi baada ya kuhukumiwa kunyongwa hatua iliyosababisha ghadhabu dunia nzima.

Aliachwa huru mwezi Juni baada ya kuwepo kwa mashinikizo.

BBC

5 comments:

Anonymous said...

tafuta pesa na umarufu bibiye mpango mzima ndo huo.

Anonymous said...

Ndugu mwandishi wa hii habari hii ukweli ni kwamba huyo mwanamke alikuwa mkristo na alishikilia msimamo wake pale alipotakiwa kubadili kuwa muislamu kwa sababu baba yake mzazi alikuwa muislamu. Baba Yale alimtelekeza akalelewa na bibi yake kizaa mama take ambaye alikuwa mkristo na ndiyo dini maishani mwake amekuwa akiabudu. Tatizo lilikuja baada ya watu kumshitaki na kulingana na sheria nchi Sudani lazima mtoto aliyezaliwa na muislamu( baba muislamu) mtoto anatakiwa naye awe muislamu.

Anonymous said...

Bro jaribu kuandika ukweli halisi huyu mama hakubadili dini bali kazaliwa na baba islam mama Christian na kaolewa na usa/s sudan Christian guy kwa maelezo yake anasema hajawahi kuwa islam sasa hii kubadili dini unapata wapi? Asilimia kubwa ya s Sudan Ni Christian ndio sbb ya usa kugawa hii nchi

Anonymous said...

Haki ya Mungu ndiyo iliyomshindania huyo dada. Asanteni serikali ya Italy na USA kwa kumsaidia mtu huyu. Vinginevyo angekuwa mhanga wa dini chinja chinja na kuua viumbe wa Mwenyezi Mungu. Sababu Mungu haabudiwi kwa makali ya upanga au kwa mtutu wa bunduki, bali kwa hiari ya mtu binafsi. Justice continue prevailing day and night.

Anonymous said...

Mtasema saana. Swala hapa si merium kuwa mkristo au katelekezwa na baba yake (mwislam)..bali ni ushenzi unaofanywa na watu wenye imani finyu na Elimu ndogo ya mawazo. Nahisi dada zetu watajifunza mengi kutokana na kitendo cha huyu dada kuwa na msimamo wakutokukubali kuyumbishwa kwa vitisho vya kunyongwa.