Advertisements

Wednesday, April 16, 2014

BREAKING NEWS:: WABUNGE WA UPINZANI WASUSA NA KUTOKA NJE YA UKUMBI WA BUNGE LA KATIBA

SHE SHE LILIANZIA HAPA....

Makamu mwenyekiti anatoa matangazo ya wageni wa wajumbe wa bunge maalum la katiba pamoja na wageni wengine waalikwa.
Anasema amepokea hati ya makubaliano ya muungano na ni certified copy.
Anamkaribisha mh. Wassira aweze kutoa neno kuhusu hati hiyo.
Mh. Steven Wassira, anasema hati hiyo ipo na ni halisi na ipo katika hali nzuri hata baada ya kusainiwa miaka hamsini iliyopita.
Anasema kuwa Tundu Lissu na wenzake walikutana baada ya kujua hati ipo na wakakubaliana waseme saini ya Sheikh Karume sio ya kweli.
Anasema watanzania tujihadhari na mawakala wa shetani.
Anasema waasisi wetu wametukanwa sana mpaka kuitwa madikteta na hali hii haivumiliki kwa watanzania wote.
Anasema heshima ya waasisi wetu hailindwi na vyama bali inalindwa na italindwa na watanzania wote.
Makamu mwenyekiti,
Bunge litaendelea Saa kumi jioni.
Anasitisha kikao cha bunge maalum la katiba.

======== Bunge Maalum la Katiba, kikao cha jioni =======
Mh.
Anaanza kwa kuunga mkono maoni ya wengi ambayo inatambua uwepo wa serikali mbili.
Anasema zanzibar kuna makundi mawili yanayotaka mkataba na serikali mbili.
Sababu za kuunga s2 ni kuwa muungano huu ni kuna kero za muda mrefu na anasema kuwa kuna kero zishatatulika.
Serikali ya tatu ya nini wakati kero zinatatulika.
Anasema kuwa s3 haijaja lakini tayari ina kero 6,yanini kuwa muungano wa s3 ambayo tayari ina kero sita wakati kero za s2 zinatatulika.
Anasema cuf imefika bara na kumezwa na ukawa,wametoka zanzibar na asilimia 65 ya serikali ya mkataba lakini walivyofika bara wakamezwa na chadema.
Anasema chadema imewapa cuf majina tofauti na cuf wamejisahau kuwa chadema ndiyo inayoibomoa zanzibar.
Anasema amiri jeshi mkuu wa tanzania ni mmoja na ni rais wa JMT hivyo tundu lissu asipotoshe.
Anasema miaka hamsini hii ya muungano hawapaswi kustuka maana mtu mzima hatishiwi nyau.

Mh. Mch. Ernest Kadiva
Anaanza kwa kumshukuru Mungu.
Anasema wanatakiwa kuunda katika ya wananchi wote na yenye misingi madhubuti ya kusimamia nchi kwa muda mrefu.
Anasema taifa linaeza kuporomoka muda wowote kama haina msingi ulio imara na hivyo msingi lazima ulindwe.
Anasema kuwa ili taifa liweze kuvunjika lazima ikatwe mizizi imara ya msingi wa taifa hivyo taifa litatetereka.
Anapendekeza kuwa JMT ni nchi inayomtambua Mungu,Isiyo na dini na isiyoruhusu uchafuzi (kashfa) za kidini.
Anasema dini ni msingi imara wa ustawi wa nchi.
Anasema kama wosia wao bado una mantiki katika muundo huu wa serikali mbili basi bora uenziwe.
Wananchi wanataka kuona uchumi ulioimarika na mfumo watakaoutaka basi uhakikishe unazingatia na namna ya kuimarisha uchumi ambacho ndo wananchi wanachotaka kuona.

Mh. Prof Lipumba
Anasema yeye ni muumini wa dini ya mwenyezi Mungu hivyo ni muumini wa mapendekezo yaliyoletwa na tume ya Warioba.
Anamnukuu Lukuvi alivyoenda kanisani na kuwaasa waumini waupinge muundo wa S3 lasi hivyo nchi itataliwa na jeshi,anasema Lukuvi aliwasilisha maoni ya Waziri mkuu.
Anasema km zanzibar wangetaka muundo wa s1 moja basi wangekuwa na muundo wa serikali moja lakini wazanzibar hawati muundo huo,anasema wanataka muungano utakaokuwa na maridhiano.
Anasema wanahitaji katiba itakayokuwa sawa kwa wananchi wote maana ndo msingi ulioachwa na mwl Nyerere.
Anasema ni fedhea kwa waziri kwenda kusema kanisani kuwa cuf zanzibar wanataka muungano utakaoifanya zanzibar kuwa nchi ya kiislam.
Anasema watatumiaje bajeti kubwa kukarabati ukumbi wakato wanajua katika hawaitaki.
Anasema wamechoka ubaguzi na kudharau maoni ya wananchi.
Anasema watu wote wanaokubaliana na maoni ya wananchi wanaondoka bungeni na kuwaacha wao wajadili katiba wanayoitaka.

Wabunge wengi wameondoka ndani ya ukumbi wa bunge na makamu mwenyekiti anasema kuwa wakati wanaanza kikao cha bunge kolamu ilikuwa imetimia hivyo kanuni inawaruhusu kuendelea na kikao.

Mh. Nyangwine Nyambari, SOURCE: JAMII FORUM

2 comments:

Anonymous said...

Hawa wapinzani jamani WANAKERA!!! WANATAKA NINI JAMANI HEMBU WATUACHIE NCHI YETU NA AMANI WASUBIRI KUOMBA KURA. DAALILI ZIMEISHAJIONYESHA KUWA WATANZANIA HAWAPO TAYARI KUIPA NCHI WATU WENYE JAZBA BORA TUFE NA HIYO CCM YETU TUTASAFISHANA TARATIIIIBU! Kweli mwl Nyerere na Karume wafanye mkataba wa kihuni?? THESE TWO GUYS WERE INTERLECTUAL NA WACHA MUNGU JAMANI MLISEMA MKATABA HAUPO, UMEPATIKANA WANASEMA SAHIHI YA KARUME SIYO. SASA TUNAANZA KUDOUBT YOU CHADEMA CREDIBILITY! MNATAKA KUPOTEZA HELA ZA WALIPA KODI AU KUTUNGA KATIBA YETU???
Mungu ibariki Tanzania.

Anonymous said...

Huu ni usaliti na tisipokuwa makini serikali ya CCM itasababisha machafuko nchini. Bunge kuweni makini unganganizi wa serikali 2 au 3 mnazotaka je hiyo kura mbona haipigwi. Msiwaburuze WaTanzania.